MTINDO UNAVYOENDELEZA MAUDHUI KATIKA NATALA

PDF version

IKISIRI

Utafiti huu unahusu jinsi mtindo unavyoendeleza maudhui katika Natala(1997) ya Kithaka Wa Mberia. Tumeshughulikia vipengele vya kimtindo vya wahusika, matumizi ya lugha na maudhui katika ujenzi na uendelezaji wa ukombozi wa wanawake katika jamii iliyotawaliwa na mfumo wa ki-ubabedume unaojitokeza katika Natala. Tumetumia nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika kuchanganulia masuala ya mwanamke, na nadharia ya umuundo kuchunguza vipengele vya kimtindo. Kazi yetu imegawanywa katika sura tano. Katika suraya kwanza tumejadili somo la utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka, nadharia tete, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Katika sura ya pili tumeshughulikia historia fupi ya tamthilia, awamu za maendeleo ya tamthilia-kipindi cha kabla ya ukoloni, kipindi cha ukoloni na baada ya ukoloni. Aidha tumeshughulikia muhtasari wa Natala. Katika sura ya tatu tumechunguza mchango wa wahusika katika ujenzi na uendelezaji wa maudhui. Tumeangazia dhana ya wahusika,wahusika wakuu na wahusika wadogo, ulinganuzi wa wahusika,umakundi wa wahusika na dhima yao katika ujenzi wa maudhui.

Sura ya nne imeshughulikia matumizi ya tamathali za usemi na kunga za fasihi na athari zake katika kuendeleza maudhui. Aidha tumechunguza mandhari yalivyohusishwa na matukio katika ujenzi na uendelezaji wa maudhui. Sura ya tano ni hitimisho la utafiti wetu. Tumejadili muhtasari wa matokeo na mapendekezo ya utafiti wa baaadaye.

 

http://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/59975

 

Message from the Dean

Het spelen van leuke spelletjes online is geweldig. Met de komst van online blackjack is dit alleen maar beter geworden.

Prof. Peter Wasamba

Dean, Faculty of Arts

Read message from the Dean

Community Outreach

Contacts

P.O BOX 19134-40123

KISUMU

Email: foa_ksmcampus@uonbi.ac.ke

Mobile:+254-719 587 997

Second Floor-East Wing

Media Center

UoN Website | UoN Repository | ICTC Website


Copyright © 2018. ICT WebTeam, University of Nairobi