UHAKIKI WA KIMAUDHUI NA KIFANI WA KIDAGAA KIMEMWOZEA

PDF version

UHAKIKI WA KIMAUDHUI NA KIFANI

WA KIDAGAA KIMEMWOZEA

 

RONO PAULINE

MUHTASARI

Tasnifu hii ilishughulikia uhakiki wa kifani na kimaudhui wa Kidagaa Kimemwozeaya Ken Walibora(2012). Tuliangalia maudhui na tulinuia kuonyesha mbinu zilizotumiwa katika kuwaumba wahusika na jinsi wahusika vijana walivyopigania kuondoa ukoloni mambo leo katika nchi ya Tomoko. Pamoja na hayo tulishughulikia nadharia tete ya uhakiki ambayo ni mhimili wa utafiti huu. Sababu za kuchagua mada piazimeelezwa. Kazi yetu iliangazia

maudhui, fani na wahusika. Kwa vile kuna njia nyingi za kuwasiri wahusika sisi tumejibana kwa wahusika wakuu, wasaidizi na wajenzi. Misingi ya nadharia za uhalisia wa kijamaa na umuundo imezingatiwa katika uhakiki wetu. Nadharia ya uhalisia wa kijamaa ni kwa mujibu wa wanafalsafa kama vile George Lukacs,

Marxim Gorky, Zandnov na wengineo. Nadharia ya umuundo ni kwa mujibu wa Ferdinand De Saussure. Nadharia hii kuchunguza vipengele vya kazi ya sanaa, jinsi vinavyohusiana hadi kuikamilisha kazi hiyo. Huangalia namna sehemu mbalimbali za kazi ya sanaa zimefungamana. Mbinu za utafiti tulizotumia ni za

maktabani ambapo tulirejelea makala mbalimbali yakiwemo majarida, tasnifu na vitabu kadha wa kadha.

 

http://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/60424

Message from the Dean

Het spelen van leuke spelletjes online is geweldig. Met de komst van online blackjack is dit alleen maar beter geworden.

Prof. Peter Wasamba

Dean, Faculty of Arts

Read message from the Dean

Community Outreach

Contacts

P.O BOX 19134-40123

KISUMU

Email: foa_ksmcampus@uonbi.ac.ke

Mobile:+254-719 587 997

Second Floor-East Wing

Media Center

UoN Website | UoN Repository | ICTC Website


Copyright © 2018. ICT WebTeam, University of Nairobi