MATUMIZI YA USONDE NAFSI NA USONDE JAMII: MTAZAMO WA UHUSIANO

PDF version

MUHTASARI

Utafiti huu umeshughulikia matumizi ya usonde nafsi na uso

nde jamii katika mawasiliano ya walimu na wanafunzi wa Kiswahili. Tumetumia nadharia ya uhusiano kwa sababu ya sifa ya usonde ya kutegemea muktadha kwenye ufasiri wa maneno yake. Vivyo hivyo tumechagua kutafitia usonde nafsi na usonde jamii ili kutathmini

wazo la Marmaridou (2000) kuwa kategoria hizi mbili za usonde zina mtagusano kiasi cha kuchukuliwa kuwa ni kategoria moja.

Utafiti huu ulifanywa kwa kutumia utafiti stahilifu kimaelezo kwa kuwa data ambayo ilikusanywa ilikuwa katika umbo la maneno tamkwa ya walimu na wanafunzi.Hatua zilizotumiwa katika ukusanyaji ni pamoja na kusikiliza, kurekodi na kuandika. Data

ilichanganuliwa kwa kutumia utaratibu wa kusimba pronomino

pamoja na hatua za uzulishaji katika utaratibu wa ufahamu katika nadharia ya uhusiano. Hatimaye utafiti huu umeshikilia kuwa

katika lugha ya Kiswahili kuna uhusiano kati ya usonde nafsi

na usonde jamii hasa katika baadhi ya matumizi ya usonde nafsi.

Kwa hivyo haipaswi kushikilia kuwa usonde nafsi na usonde jamii ni kategoria moja ya usonde.

 

http://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/60247

Message from the Dean

Het spelen van leuke spelletjes online is geweldig. Met de komst van online blackjack is dit alleen maar beter geworden.

Prof. Peter Wasamba

Dean, Faculty of Arts

Read message from the Dean

Community Outreach

Contacts

P.O BOX 19134-40123

KISUMU

Email: foa_ksmcampus@uonbi.ac.ke

Mobile:+254-719 587 997

Second Floor-East Wing

Media Center

UoN Website | UoN Repository | ICTC Website


Copyright © 2018. ICT WebTeam, University of Nairobi